Posts

Ally Kamwe kuchukuliwa Hatua

Image
Kupitia sheria na kanuni zilizowekwa za Bodi ya Ligi kuhusu udhibiti wa viongozi huenda Afisa Habari wa klabu ya Young Africans Ali Kamwe akafungiwa miezi mitatu kujihusisha na soka, endapo sheria zitafuatwa baada ya kumfananisha Kocha Msaidizi wa Simba SC Juma Mgunda na Andazi mbele ya Mashabiki wa Young Africans. Kwa mujibu wa Kanuni nambari 46 : udhibiti wa viongozi kifungu nambari 8 kinamfunga Ally Kamwe kwa maneno ya kashfa na dhihaka kwa Juma Mgunda, na mbaya zaidi aliyatoa hadharani na kunukuliwa na vyombo vya habari. Kanuno hiyo inasema: “Kiongozi Akitoa matamshi au ishara za matusi dhidi ya mashabiki, akitoa matamshi, ishara za matusi yenye nia ya kumdhalilisha kiongozi mbele ya jamii awe wa TFF, Klabu au Taifa atatozwa faini ya shilingi milioni moja 1,000,000/- na kufungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu (3). #TotalEnergiesCAFCC #NestoShayoUPDATES #SimbaSC #yangasc  

HII HAPA MIEZI MINNE YA MUDATHIR YAHAYA NA MAAJABU YAKE NDANI YA YANGA….APEWE MAUA YAKE TU

Image
  Wakati akisajiliwa Yanga katika dirisha dogo la usajili lililodumu kwa mwezi mmoja kuanzia Disemba mwaka jana hadi Januari mwaka huu, Mudathir Yahya hakuonekana kama angeweza kupenya ndani ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kuachana na Azam FC pindi msimu uliopita ulipomalizika Juni, mwaka jana. Uwepo wa nyota wa safu ya kiungo ambao walikuwa wanafanya vizuri katika kikosi cha Yanga wakati Mudathir anasajiliwa akina Khalid Aucho, Stephane Aziz Ki, Yannick Bangala na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ ulionekana ungekuwa kikwazo kwa kiungo huyo wa Taifa Stars kupata nafasi kikosi cha kwanza. Hata hivyo, mambo yamekuwa tofauti na Mudathir ndio ameonekana kujihakikishia nafasi kikosi cha Yanga huku akiwa kipenzi cha kocha Nasreddine Nabi na benchi lake la ufundi. NGUZO LIGI KUU Tangu alipojiunga na Yanga hadi sasa, Mudathir amecheza mechi zote kumi za Ligi Kuu ambazo timu hiyo imecheza mara nyingi akiwemo katika kikosi cha kwanza huku mara kadhaa akii

KISA YANGA KUTINGA FAINAL CAF…MANARA AANIKA SIRI SABABU YA SIMBA KUISHIA ROBO FAINAL KILA MWAKA.

Image
  Aliyewahi kuwa Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Sunday Manara amesema kuwa jambo linaloiponza timu hiyo na kuishia robo fainali ya michuano ya CAF kila mwaka ni kujiona wao wakubwa kuliko timu nyingine hapa nchini na hata zile wanazokutaka nazo kimataifa. Manara amesema hayo mara baada ya Yanga kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuifunga Marumo Gallants ya Afrika Kusini huku Simba kwa miaka minne wakikomea robo fainali. “Nilikuwepo Afrika kipindi kile nilipokuwa Kolo (Asante Mungu kunivua) tuliamini tunakwenda Semi final kirahisi Coz Kaizer Chiefs ilikuwa taabani. “Maandalizi yetu yalikuwa ya hovyo, kambini kulijaa Confidence ya ajabu, matokeo yake kuingia uwanjani tukala ARBAA. “Tofauti na huku Yanga, pamoja na Marumo kuwa hoi kwenye ligi ya kwao, hatukuwadharau na tulijua wanafanya vizuri kwenye Kombe la Shirikisho. “Tulijua wanacheza ligi bora, tukaendelea kuwaheshimu hata baada ya kuwafunga mechi ya kwanza Dar, ugenini tukaja na plan ya kucheza kwa kuwaheshimu

Haji Manara Amchana Vibaya Fei Toto Baada ya Kuomba Michango ili Aende Mahakama ya CAS

Image
  Baada ya juhudi za Mchezaji Feisal Salum “Fei Toto” kugonga mwamba mara mbili TFF kwa kushindwa kukubaliwa ombi lake la kuvunja mkataba na Yanga, Mchezaji huyu leo ametangaza kuomba msaada wa pesa kwa Watanzania ili aweze kwenda kwenye Mahakama ya usuluhishi wa kimichezo (CAS). Feisal ameandika yafuatayo katika taarifa yake “Ndugu zangu Watanzania na familia yote ya soka kwa Bara na visiwani. Mimi kijana wenu ambaye kwa miaka yote nimekua na nidhamu nje na ndani ya uwanja na kwa dhati nimeitumikia klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania na Zanzibar Heroes” “Utiifu wangu umekua shubiri ya maisha yangu ya soka, nimevumilia nimeshindwa, sitamani tena mama yangu kutukanwa. TFF imeshindwa kunisaidia kupata haki yangu ya Kuvunja mkataba na Yanga hivyo nimeamua Kwenda Mahakama ya michezo CAS, nahitaji mchango wa kila Mtanzania mpenda haki na maendeleo ya Wachezaji wa Kitanzania ambao wamekua kimya na woga juu ya maslahi, heshima na haki zao.... naomba unichangie kadiri utakavyoweza ili

Fei Toto Avunja Ukimya Aomba Watanzania Wamchangie Aende Mahakama ya Michezo (CAS)

Image
  Baada ya juhudi za Mchezaji Feisal Salum “Fei Toto” kugonga mwamba mara mbili TFF kwa kushindwa kukubaliwa ombi lake la kuvunja mkataba na Yanga, Mchezaji huyu leo ametangaza kuomba msaada wa pesa kwa Watanzania ili aweze kwenda kwenye Mahakama ya usuluhishi wa kimichezo (CAS). Feisal ameandika yafuatayo katika taarifa yake “Ndugu zangu Watanzania na familia yote ya soka kwa Bara na visiwani. Mimi kijana wenu ambaye kwa miaka yote nimekua na nidhamu nje na ndani ya uwanja na kwa dhati nimeitumikia klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania na Zanzibar Heroes” “Utiifu wangu umekua shubiri ya maisha yangu ya soka, nimevumilia nimeshindwa, sitamani tena mama yangu kutukanwa. TFF imeshindwa kunisaidia kupata haki yangu ya Kuvunja mkataba na Yanga hivyo nimeamua Kwenda Mahakama ya michezo CAS, nahitaji mchango wa kila Mtanzania mpenda haki na maendeleo ya Wachezaji wa Kitanzania ambao wamekua kimya na woga juu ya maslahi, heshima na haki zao.... naomba unichangie kadiri utakavyoweza ili

YANGA WATAKA BILIONI 5 KUMUUZA MAYELE…MAMELOD, AL HILAL NA MAZEMBE KUTUMA OFA NONO ZAIDI

Image
  Wakati tetesi zikisambaa kila kona kuhitajika nwa Vilabu vingi Barani Afrika kwa Mshambualiaji wa Yanga Fiston Mayele. Afisa wa habari wa Yanga Ali Kamwe amevikaribisha vilabu vyote ambavyo vinamtaka mshambuliaji wao Fiston kalala Mayele waje wakae mezani wamalizane. “Sisi Kama Yanga hatuwezi kumzuia Fiston kalala Mayele kwenda sehemu nyingine Ila thamani ya Fiston kalala Mayele kwa sasa ni Billion 5 kuvunja mkataba wake watu wasiogope hata mwakarobo Kama wanamuhitaji waje tumalizane tunachotaka tu utaratibu ufatwe”. Tayari klabu ya Mamelod Sundowns ya Afrika ya kusini imeweka wazi nia yake ya kutaka kumsajili Mayele kwa ajili ya kuimarisha safi yao ya ushambuliaji kwa  msimu ujao. Hata hivyo, taarifa kutoka Sudani pia zinadai kuwa klabu ya Al Hilal inayonolewa na Mkongomani Frorent Ibenge nayo imeonyesha nia ya kumtaka mshambuliaji huyo. Inaelezwa kuwa, maafisa wa Al Hilal walianza kumtupia macho Mayele baada ya mechi yao ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika

TP Mazembe imepokea ofa rasmi kutoka Ulaya kwa Jean Baleke, imethibitishwa 100%

Image
  | ππ‘π„π€πŠπˆππ†: ◉ TP Mazembe has received an official offer from Europe for Jean Baleke, confirmed 100%. ◉ The club that submitted the offer played in Europa League group stage this season and next year, they will play in the UEFA Champions League. ◉ The contract offered is three-years. ◉ Simba has been informed by this offer and are aware now. ◉ Baleke’s camp has been very respectful since the player has one more year loan deal with the Tanzanian giants. ◉ “Baleke want to go and get a chance of his life” his agent tells me. ◉ There’s a meeting arranged by all parties once the season end in Tanzania. ◉ Baleke will leave Simba at the end of the season if all goes to plan. Here: The right news only. IN SWAHILI: | ππ‘π„π€πŠπˆππ†: ◉ TP Mazembe imepokea ofa rasmi kutoka Ulaya kwa Jean Baleke, imethibitishwa 100%. ◉ Klabu iliyowasilisha ofa hiyo ilicheza hatua ya makundi ya Ligi ya Europa msimu huu na mwaka ujao, itacheza Ligi ya Mabingwa ya UEFA. ◉ Mkataba unaotolewa ni wa miaka m