Ally Kamwe kuchukuliwa Hatua

Kupitia sheria na kanuni zilizowekwa za Bodi ya Ligi kuhusu udhibiti wa viongozi huenda Afisa Habari wa klabu ya Young Africans Ali Kamwe akafungiwa miezi mitatu kujihusisha na soka, endapo sheria zitafuatwa baada ya kumfananisha Kocha Msaidizi wa Simba SC Juma Mgunda na Andazi mbele ya Mashabiki wa Young Africans.



Kwa mujibu wa Kanuni nambari 46 : udhibiti wa viongozi kifungu nambari 8 kinamfunga Ally Kamwe kwa maneno ya kashfa na dhihaka kwa Juma Mgunda, na mbaya zaidi aliyatoa hadharani na kunukuliwa na vyombo vya habari.

Kanuno hiyo inasema: “Kiongozi Akitoa matamshi au ishara za matusi dhidi ya mashabiki, akitoa matamshi, ishara za matusi yenye nia ya kumdhalilisha kiongozi mbele ya jamii awe wa TFF, Klabu au Taifa atatozwa faini ya shilingi milioni moja 1,000,000/- na kufungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu (3). #TotalEnergiesCAFCC #NestoShayoUPDATES #SimbaSC #yangasc  

Comments

Popular posts from this blog

Lavalava kujiunga na Aftermath Entertainment na kuondoka WCB

Kundi la Sauti Soul Kuvunjika

BAADA YA KUWA ‘MNYONGE SANA’ …PHIRI KUWA CHINI YA UANGALIZI MAALUMU SIMBA