Rema, Ayra Starr watishia ufalme wa Diamond Platnumz
Ikumbukwe hata video za Diamond ambazo zimefikisha 'views' milioni 100, hakuna iliyofanya hivyo ndani ya mwaka mmoja ila Rema kafanya hivyo mara nne yake tena kwa miezi 12 tu. Rema ndiye msanii wa kwanza Afrika kufanya hivyo wakati rekodi ya Diamond ni Kusini mwa Jangwa la Sahara tu. Remix ya wimbo huo ambayo Rema kamshirikisha Selena Gomez, video yake iliachiwa Septemba 7, 2022 na ndani ya miezi saba sasa tayari imefikisha 'views' milioni 358. Kwa mwaka 2022 Rema alikuwa ndiye mwanamuziki aliyefanya vizuri zaidi YouTube Afrika wakati Diamond hakuwa hata ndani ya 10 bora!. Rema ndiye alichukua nafasi ya kwanza na ya pili katika orodha ya video 10 zilizotazamwa zaidi YouTube Afrika 2022, video nyingine ni Last Last ya Burna Boy (mil. 140), Buga ya Kizz Daniel (mil. 108) na For My Hand ya Burna Boy (mil. 70). Nyingine ni Finesse ya Pheelz (mil. 61), Emiliana ya Ckay (mil. 57), Ku Lo Sa ya Oxlade (mil. 54), No Wahala Remix ya 1da Banton (mil. 53) na Rush ya Ayra Starr (mil