Posts

Showing posts from May, 2023

Ally Kamwe kuchukuliwa Hatua

Image
Kupitia sheria na kanuni zilizowekwa za Bodi ya Ligi kuhusu udhibiti wa viongozi huenda Afisa Habari wa klabu ya Young Africans Ali Kamwe akafungiwa miezi mitatu kujihusisha na soka, endapo sheria zitafuatwa baada ya kumfananisha Kocha Msaidizi wa Simba SC Juma Mgunda na Andazi mbele ya Mashabiki wa Young Africans. Kwa mujibu wa Kanuni nambari 46 : udhibiti wa viongozi kifungu nambari 8 kinamfunga Ally Kamwe kwa maneno ya kashfa na dhihaka kwa Juma Mgunda, na mbaya zaidi aliyatoa hadharani na kunukuliwa na vyombo vya habari. Kanuno hiyo inasema: “Kiongozi Akitoa matamshi au ishara za matusi dhidi ya mashabiki, akitoa matamshi, ishara za matusi yenye nia ya kumdhalilisha kiongozi mbele ya jamii awe wa TFF, Klabu au Taifa atatozwa faini ya shilingi milioni moja 1,000,000/- na kufungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu (3). #TotalEnergiesCAFCC #NestoShayoUPDATES #SimbaSC #yangasc  

HII HAPA MIEZI MINNE YA MUDATHIR YAHAYA NA MAAJABU YAKE NDANI YA YANGA….APEWE MAUA YAKE TU

Image
  Wakati akisajiliwa Yanga katika dirisha dogo la usajili lililodumu kwa mwezi mmoja kuanzia Disemba mwaka jana hadi Januari mwaka huu, Mudathir Yahya hakuonekana kama angeweza kupenya ndani ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kuachana na Azam FC pindi msimu uliopita ulipomalizika Juni, mwaka jana. Uwepo wa nyota wa safu ya kiungo ambao walikuwa wanafanya vizuri katika kikosi cha Yanga wakati Mudathir anasajiliwa akina Khalid Aucho, Stephane Aziz Ki, Yannick Bangala na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ ulionekana ungekuwa kikwazo kwa kiungo huyo wa Taifa Stars kupata nafasi kikosi cha kwanza. Hata hivyo, mambo yamekuwa tofauti na Mudathir ndio ameonekana kujihakikishia nafasi kikosi cha Yanga huku akiwa kipenzi cha kocha Nasreddine Nabi na benchi lake la ufundi. NGUZO LIGI KUU Tangu alipojiunga na Yanga hadi sasa, Mudathir amecheza mechi zote kumi za Ligi Kuu ambazo timu hiyo imecheza mara nyingi akiwemo katika kikosi cha kwanza huku mara kadhaa akii

KISA YANGA KUTINGA FAINAL CAF…MANARA AANIKA SIRI SABABU YA SIMBA KUISHIA ROBO FAINAL KILA MWAKA.

Image
  Aliyewahi kuwa Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Sunday Manara amesema kuwa jambo linaloiponza timu hiyo na kuishia robo fainali ya michuano ya CAF kila mwaka ni kujiona wao wakubwa kuliko timu nyingine hapa nchini na hata zile wanazokutaka nazo kimataifa. Manara amesema hayo mara baada ya Yanga kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuifunga Marumo Gallants ya Afrika Kusini huku Simba kwa miaka minne wakikomea robo fainali. “Nilikuwepo Afrika kipindi kile nilipokuwa Kolo (Asante Mungu kunivua) tuliamini tunakwenda Semi final kirahisi Coz Kaizer Chiefs ilikuwa taabani. “Maandalizi yetu yalikuwa ya hovyo, kambini kulijaa Confidence ya ajabu, matokeo yake kuingia uwanjani tukala ARBAA. “Tofauti na huku Yanga, pamoja na Marumo kuwa hoi kwenye ligi ya kwao, hatukuwadharau na tulijua wanafanya vizuri kwenye Kombe la Shirikisho. “Tulijua wanacheza ligi bora, tukaendelea kuwaheshimu hata baada ya kuwafunga mechi ya kwanza Dar, ugenini tukaja na plan ya kucheza kwa kuwaheshimu

Haji Manara Amchana Vibaya Fei Toto Baada ya Kuomba Michango ili Aende Mahakama ya CAS

Image
  Baada ya juhudi za Mchezaji Feisal Salum “Fei Toto” kugonga mwamba mara mbili TFF kwa kushindwa kukubaliwa ombi lake la kuvunja mkataba na Yanga, Mchezaji huyu leo ametangaza kuomba msaada wa pesa kwa Watanzania ili aweze kwenda kwenye Mahakama ya usuluhishi wa kimichezo (CAS). Feisal ameandika yafuatayo katika taarifa yake “Ndugu zangu Watanzania na familia yote ya soka kwa Bara na visiwani. Mimi kijana wenu ambaye kwa miaka yote nimekua na nidhamu nje na ndani ya uwanja na kwa dhati nimeitumikia klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania na Zanzibar Heroes” “Utiifu wangu umekua shubiri ya maisha yangu ya soka, nimevumilia nimeshindwa, sitamani tena mama yangu kutukanwa. TFF imeshindwa kunisaidia kupata haki yangu ya Kuvunja mkataba na Yanga hivyo nimeamua Kwenda Mahakama ya michezo CAS, nahitaji mchango wa kila Mtanzania mpenda haki na maendeleo ya Wachezaji wa Kitanzania ambao wamekua kimya na woga juu ya maslahi, heshima na haki zao.... naomba unichangie kadiri utakavyoweza ili

Fei Toto Avunja Ukimya Aomba Watanzania Wamchangie Aende Mahakama ya Michezo (CAS)

Image
  Baada ya juhudi za Mchezaji Feisal Salum “Fei Toto” kugonga mwamba mara mbili TFF kwa kushindwa kukubaliwa ombi lake la kuvunja mkataba na Yanga, Mchezaji huyu leo ametangaza kuomba msaada wa pesa kwa Watanzania ili aweze kwenda kwenye Mahakama ya usuluhishi wa kimichezo (CAS). Feisal ameandika yafuatayo katika taarifa yake “Ndugu zangu Watanzania na familia yote ya soka kwa Bara na visiwani. Mimi kijana wenu ambaye kwa miaka yote nimekua na nidhamu nje na ndani ya uwanja na kwa dhati nimeitumikia klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania na Zanzibar Heroes” “Utiifu wangu umekua shubiri ya maisha yangu ya soka, nimevumilia nimeshindwa, sitamani tena mama yangu kutukanwa. TFF imeshindwa kunisaidia kupata haki yangu ya Kuvunja mkataba na Yanga hivyo nimeamua Kwenda Mahakama ya michezo CAS, nahitaji mchango wa kila Mtanzania mpenda haki na maendeleo ya Wachezaji wa Kitanzania ambao wamekua kimya na woga juu ya maslahi, heshima na haki zao.... naomba unichangie kadiri utakavyoweza ili

YANGA WATAKA BILIONI 5 KUMUUZA MAYELE…MAMELOD, AL HILAL NA MAZEMBE KUTUMA OFA NONO ZAIDI

Image
  Wakati tetesi zikisambaa kila kona kuhitajika nwa Vilabu vingi Barani Afrika kwa Mshambualiaji wa Yanga Fiston Mayele. Afisa wa habari wa Yanga Ali Kamwe amevikaribisha vilabu vyote ambavyo vinamtaka mshambuliaji wao Fiston kalala Mayele waje wakae mezani wamalizane. “Sisi Kama Yanga hatuwezi kumzuia Fiston kalala Mayele kwenda sehemu nyingine Ila thamani ya Fiston kalala Mayele kwa sasa ni Billion 5 kuvunja mkataba wake watu wasiogope hata mwakarobo Kama wanamuhitaji waje tumalizane tunachotaka tu utaratibu ufatwe”. Tayari klabu ya Mamelod Sundowns ya Afrika ya kusini imeweka wazi nia yake ya kutaka kumsajili Mayele kwa ajili ya kuimarisha safi yao ya ushambuliaji kwa  msimu ujao. Hata hivyo, taarifa kutoka Sudani pia zinadai kuwa klabu ya Al Hilal inayonolewa na Mkongomani Frorent Ibenge nayo imeonyesha nia ya kumtaka mshambuliaji huyo. Inaelezwa kuwa, maafisa wa Al Hilal walianza kumtupia macho Mayele baada ya mechi yao ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika

TP Mazembe imepokea ofa rasmi kutoka Ulaya kwa Jean Baleke, imethibitishwa 100%

Image
  | 𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆: ◉ TP Mazembe has received an official offer from Europe for Jean Baleke, confirmed 100%. ◉ The club that submitted the offer played in Europa League group stage this season and next year, they will play in the UEFA Champions League. ◉ The contract offered is three-years. ◉ Simba has been informed by this offer and are aware now. ◉ Baleke’s camp has been very respectful since the player has one more year loan deal with the Tanzanian giants. ◉ “Baleke want to go and get a chance of his life” his agent tells me. ◉ There’s a meeting arranged by all parties once the season end in Tanzania. ◉ Baleke will leave Simba at the end of the season if all goes to plan. Here: The right news only. IN SWAHILI: | 𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆: ◉ TP Mazembe imepokea ofa rasmi kutoka Ulaya kwa Jean Baleke, imethibitishwa 100%. ◉ Klabu iliyowasilisha ofa hiyo ilicheza hatua ya makundi ya Ligi ya Europa msimu huu na mwaka ujao, itacheza Ligi ya Mabingwa ya UEFA. ◉ Mkataba unaotolewa ni wa miaka m

KISA Cha Kusikitisha 'Baba Yangu Alisababisha Nilale na Mjomba Wangu, Kamwe Sitamsamehe'

Image
  Nimeona leo nitoe siri yangu hapa ya muda mrefu ambayo imekuwa ikiniumiza sana pale tu ninapokumbuka, nakosa raha na amani inapotea. Kwa ufupi kabisa, nilizaliwa mkoani Mara wilaya ya Musoma mjini maeneo ya Nyakato, mama yangu alibeba mimba yangu akiwa darasa sita hivyo hakumaliza shule. Ilibidi akae nyumbani mpaka pale alipojifungua, kwa wakati kulikuwa hakuna sheria kali kwa wanaowapatia wanafunzi mimba wakiwa shule. Na aliyempatia hiyo mimba naye alikuwa mwanafunzi mwenzake lkn alikuwa la saba yeye alimaliza shule. Baba yake mama ambaye ni babu yangu alikuwa na uwezo mkubwa hivyo hakushindwa kutulea mimi na mama. Nikiwa na miaka 6 ndipo nilipokuja kumjua baba yangu wakati huo nae alikuwa amekuwa mtu mzima, alikuja akanisalimia akaondoka, kwao pia walikuwa vizuri kimaisha. Nikiwa na miaka 9 naanza darasa la kwanza wakati huo tulikuwa tunaingia shule tukiwa na umri mkubwa tofauti na sasa. Mama aliolewa na mume mwingine na alikuwa ni askari jeshi, alifanikiwa kuzaa nae watoto wanne j

Mayele Hauzwi, Yanga Yaweka Masharti Maguma

Image
  UONGOZI wa Yanga umetamka kuwa mshambuliaji wao Mkongomani Fiston Mayele hayupo sokoni lakini wapo tayari kukaa meza moja kwa klabu zinazomuhitaji kwa ajili ya mazungumzo. Aliongeza kuwa kabla ya kuanza mazungumzo hayo ya Mayele na hizo klabu, kikubwa wafahamu kuwa dau la Mayele hivi sasa linafikia zaidi ya Sh 5Bil ambazo zitawashawishi wao wamuachie mshambuliaji huyo. #Yanga #Mayele #AZIZK

Majembe Saba Yaipa Kicheko Simba Katika Orodha Ya Kuwania Tuzo

Image
MAJEMBE saba yanayovuja jasho la haki ndani ya kikosi cha Simba yamewapa kicheko Simba wakiamini kuwa hawajabahatisha kupenya kwenye orodha ya kuwania tuzo bali ubora umewababe. Katika orodha ya kuwania tuzo ndani ya ligi msimu wa 2022/23 tayari Kamati ya Tuzo Tanzania iliyo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) imetaja mastaa waliopenya kuwania tuzo zinazotarajiwa kufanyika hivi karibuni huku Simba ikitoa mastaa saba. Ni kwenye kipengele cha mchezaji bora ni nyota wawili wamepenya ambao ni Mzamiru Yassin na Saido Ntibanzokiza wote ni viungo. Aishi Manula maarufu kama Air Manula kipa namba moja wa timu hiyo amepenya kwenye kuwania tuzo ya kipa bora akipambana na Djigui Diarra wa Yanga na Benedict Haule wa Singida Big Stars. Watatu wamepenya kwenye tuzo ya beki bora ambao ni Shomari Kapombe, Henock Inonga na Mohamed Hussein sawa na watatu waliopenya kuwania tuzo ya kiungo bora ikiwa ni Clatous Chama, Mzamiru na Sadio. Wakati wachezaji wao wakipenya na jina la kocha Roberto Oliveir

BAADA YA KUWATAZAMA YANGA…KOCHA WA USM ALGER KANUGA WEE..KISHA AKASEMA HAYA

Image
  Kocha Mkuu wa USM Alger ya Algeria, Abdelhak Benchikha amesema hana hofu na kiwango cha Yanga na wategemee mechi ngumu zaidi ya zote zilizopita kwani wanahitaji kombe hili. “Wanatakiwa kufahamu kuwa wanakwenda kukutana na timu ya tofauti kuliko walizokutana nazo katika hatua waliyocheza,tunalihitaji hili kombe,tunaheshimu uwezo wao,” Kocha USM ALGER, Abdelhak Benchikha. Yanga atakutana na USM, Jumapili ijayo, Mei 28, 2023 katika mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa katika Dimba la Mkapa jijini dar es Salaam na mchezo wa pili utapigwa Algeria Juni 4. USM ALger imetinga fainali ya michuano hiyo kwa kuiondoa AS FAR Rabat ya Morocco kwa jumla ya mabao 4-3 huku Yanga ikiiondoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 4-1.

BAADA YA KUWA ‘MNYONGE SANA’ …PHIRI KUWA CHINI YA UANGALIZI MAALUMU SIMBA

Image
  Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Moses Phiri yupo mikononi mwa Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliveira kutokana na kupewa program maalumu itakayomrejesha kwenye ubora wake. Desemba 21, mwaka jana, Phiri alipata maumivu ya mguu kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba walipotoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1. Baada ya hapo amekuwa nje akipambania hali yake na hata aliporejea uwanjani Februari 11, 2023 Uwanja wa General Lansana Conte dhidi ya Horoya alitumia dakika 29 alikwama kurejea kwenye hali yake ya kucheka na nyavu. Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally amesema Phiri ana program maalumu itakayomrejesha kwenye ubora, na msimu ujao atakuwa tayari kuipambania timu. “Phiri alikuwa bado hajawa fiti baada ya kupata maumivu alipokuwa kwenye majukumu yake ya kazi ila kwa sasa ana program maalumu ambayo itamfanya arejee kwenye ubora. “Ni matumaini yetu atakuwa fiti tayari kwa kuwapa furaha Wanasimba hivyo muhimu kuwa na subra kila kitu kitakuwa sawa

KUHUSU MZIGO AMBAO SIMBA NA YANGA ZITAPA CAF…UKWELI HUU HAPA…PESA ZAONGEZWA

Image
Simba imeng’olewa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, lakini taarifa njema kwano ni kule kuongezwa mkwanja ikijihakikisha kuvuna Dola 900,000 (zaidi ya Sh 2 Bilioni) baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuongeza mzigo wa fedha za zawadi kwa michuano ya msimu huu. Ongezeko hilo la fedha halijainufaisha Simba tu, bali hadi watani wao, Yanga ambao imetinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwani hadi sasa ina uhakika wa kuvuta Dola 1 Milioni (zaidi ya Sh 2.35 Bilioni, badala ya 1.8 Bilioni zilizokuwa kwenye kiwango cha zawadi cha awali ikimaliza ya pili. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi jioni kwenye mtandao wa CAF, ni kwamba zawadi za msimu huu zimeboreshwa kwa asilimia 40 ikiwa ni utekelezaji wa ratifa zilizowahi kutolewa na Rais wa Shirikisho hilo, Dk Patrice Motsepe mapema mwaka huu juu ya ongezeko hilo. Kwa mujibu wa viwango vya sasa vya zawadi hizo kwa Ligi ya Mabingwa, Bingwa anazoa Dola 4 Milioni (zaidi ya Sh 9.4 Bilioni), huku anayemaliza wa p

Rema, Ayra Starr watishia ufalme wa Diamond Platnumz

Image
Ikumbukwe hata video za Diamond ambazo zimefikisha 'views' milioni 100, hakuna iliyofanya hivyo ndani ya mwaka mmoja ila Rema kafanya hivyo mara nne yake tena kwa miezi 12 tu. Rema ndiye msanii wa kwanza Afrika kufanya hivyo wakati rekodi ya Diamond ni Kusini mwa Jangwa la Sahara tu. Remix ya wimbo huo ambayo Rema kamshirikisha Selena Gomez, video yake iliachiwa Septemba 7, 2022 na ndani ya miezi saba sasa tayari imefikisha 'views' milioni 358. Kwa mwaka 2022 Rema alikuwa ndiye mwanamuziki aliyefanya vizuri zaidi YouTube Afrika wakati Diamond hakuwa hata ndani ya 10 bora!. Rema ndiye alichukua nafasi ya kwanza na ya pili katika orodha ya video 10 zilizotazamwa zaidi YouTube Afrika 2022, video nyingine ni Last Last ya Burna Boy (mil. 140), Buga ya Kizz Daniel (mil. 108) na For My Hand ya Burna Boy (mil. 70). Nyingine ni Finesse ya Pheelz (mil. 61), Emiliana ya Ckay (mil. 57), Ku Lo Sa ya Oxlade (mil. 54), No Wahala Remix ya 1da Banton (mil. 53) na Rush ya Ayra Starr (mil

Huyu Ndio Mwamuzi wa Mechi ya Kwanza Fainali Yanga na USM Alger"

Image
CONFIRMED: Mwamuzi Jean-Jacques Ngambo Ndala kutoka DR Congo 🇨🇩 ndiye atakayeamua dakika 90 za mechi ya kwanza ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika kati ya YANGA na USM ALGER Mei 28 katika dimba la Mkapa saa 10:00 jioni.

Tuache Unafiki...Simba Mchawi Wenu Msimu Huu ni Huyu Hapa

Image
Simba Pengine hizi zitabaki kuwa ni fikra zangu tu! Lakini yote ilikuwa ni usajiri tu! Ukiitizama Yanga SC ambayo iliwachukuwa takribani miaka 5 hadi 4 kurudi katika ubora wake na kushinda mataji mbele ya Simba na Azam, ilikuwa ni usajiri tu! Kipindi kile Simba anashinda mataji ya Ligi Kuu Mara 4 mfululizo mbele ya Yanga SC, ilikuwa ni usajili tu! Kule Yanga kulikuwa na usajili usiyoendana na ukubwa wa klabu, pia ulikuwa haulingani ubora na mahasimu wao ambao ni Simba wakionekana ni bora kila idara na kushinda mataji mara 4 kwa sababu Simba walikuwa na usajiri bora kuliko watani zao Yanga, ilikuwa ni usajiri tu! Simba kulikuwa na akina kachi kahata, Louis Miquissone, Chama, Meddie Kagere, John Bocco, Hassan Dilunga, Emmanuel Okwi, Deo Kanda, Gyan na wengine. Wote wakiwa kwenye ubora na wakiitumikia Simba kwa faida kubwa, wengine wakauzwa, wengine wakabaki, na wengine wakaachwa, yote ilikuwa ni usajiri tu! Kule Yanga kulikuwa na akina Sadney Urikhob, Lamine Moro, Juma Balinya, Yikpe, D