Lavalava kujiunga na Aftermath Entertainment na kuondoka WCB

Hakuna ubishi kuwa baada ya Mbosso na Zuchu kusainiwa kulipelekea WCB Wasafi kupunguza nguvu kwa baadhi ya wasanii ambao ni Lava Lava na na Queen Darleen.


Mathalani ni zaidi ya miaka mitatu sasa Queen Darleen hajatoa wimbo, mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa Aprili 2020 alipoachia ngoma, Bachela akimshirikisha Lava Lava, huku akiwa hajatoa albamu wala EP chini ya WCB Wasafi.

Ujio wa wageni hao wawili hasa Zuchu, kunaweza kutafsiriwa kama kutia mchanga kitumbua cha Lava Lava, mfano Zuchu amekuwa anatoa ngoma mfululizo kuliko msanii yoyote wa WCB Wasafi.

Wakati Lava Lava anatimiza miezi tisa bila kutoa ngoma, kwa kipindi hicho Zuchu ameweza kutoa ngoma sita ambazo ni Jaro, Love, Kwikwi, Utaniua, Napambana na Nani.

Kwa mwenendo huo huwenda maisha ya Lava Lava sio marefu ndani ya WCB Wasafi, anaweza kuondoka kama ilivyokuwa kwa Harmonize, Rich Mavoko na Rayvanny.

Hata hivyo, swali la wengi ni vipi ataweza kupata mafanikio kuzidi yale aliyopata chini ya lebo hiyo? au ataenda kuwa tishio kama Eve baada ya kuachana na Aftermath Entertainment?

Mwisho.

#avmediaupdates #avmediainfos #breaknews #radio #vpl #epl #tmz #netflix #tv #youtube #habari #bongofleva #bongomovie #muziki #movie #Tanzania #Kenya #uganda #burundi #rwanda

Comments

Popular posts from this blog

Kundi la Sauti Soul Kuvunjika

BAADA YA KUWA ‘MNYONGE SANA’ …PHIRI KUWA CHINI YA UANGALIZI MAALUMU SIMBA