KISA Cha Kusikitisha 'Baba Yangu Alisababisha Nilale na Mjomba Wangu, Kamwe Sitamsamehe'
Nimeona leo nitoe siri yangu hapa ya muda mrefu ambayo imekuwa ikiniumiza sana pale tu ninapokumbuka, nakosa raha na amani inapotea. Kwa ufupi kabisa, nilizaliwa mkoani Mara wilaya ya Musoma mjini maeneo ya Nyakato, mama yangu alibeba mimba yangu akiwa darasa sita hivyo hakumaliza shule. Ilibidi akae nyumbani mpaka pale alipojifungua, kwa wakati kulikuwa hakuna sheria kali kwa wanaowapatia wanafunzi mimba wakiwa shule. Na aliyempatia hiyo mimba naye alikuwa mwanafunzi mwenzake lkn alikuwa la saba yeye alimaliza shule. Baba yake mama ambaye ni babu yangu alikuwa na uwezo mkubwa hivyo hakushindwa kutulea mimi na mama. Nikiwa na miaka 6 ndipo nilipokuja kumjua baba yangu wakati huo nae alikuwa amekuwa mtu mzima, alikuja akanisalimia akaondoka, kwao pia walikuwa vizuri kimaisha. Nikiwa na miaka 9 naanza darasa la kwanza wakati huo tulikuwa tunaingia shule tukiwa na umri mkubwa tofauti na sasa. Mama aliolewa na mume mwingine na alikuwa ni askari jeshi, alifanikiwa kuzaa nae watoto wanne j