Rema, Ayra Starr watishia ufalme wa Diamond Platnumz



Ikumbukwe hata video za Diamond ambazo zimefikisha 'views' milioni 100, hakuna iliyofanya hivyo ndani ya mwaka mmoja ila Rema kafanya hivyo mara nne yake tena kwa miezi 12 tu. Rema ndiye msanii wa kwanza Afrika kufanya hivyo wakati rekodi ya Diamond ni Kusini mwa Jangwa la Sahara tu.

Remix ya wimbo huo ambayo Rema kamshirikisha Selena Gomez, video yake iliachiwa Septemba 7, 2022 na ndani ya miezi saba sasa tayari imefikisha 'views' milioni 358. Kwa mwaka 2022 Rema alikuwa ndiye mwanamuziki aliyefanya vizuri zaidi YouTube Afrika wakati Diamond hakuwa hata ndani ya 10 bora!.

Rema ndiye alichukua nafasi ya kwanza na ya pili katika orodha ya video 10 zilizotazamwa zaidi YouTube Afrika 2022, video nyingine ni Last Last ya Burna Boy (mil. 140), Buga ya Kizz Daniel (mil. 108) na For My Hand ya Burna Boy (mil. 70).

Nyingine ni Finesse ya Pheelz (mil. 61), Emiliana ya Ckay (mil. 57), Ku Lo Sa ya Oxlade (mil. 54), No Wahala Remix ya 1da Banton (mil. 53) na Rush ya Ayra Starr (mil. 52).

Hata hivyo, kwa Diamond mambo yalikuwa tofauti kabisa, video yake iliyofanya vizuri zaidi ni ya wimbo 'Mtasubiri' akimshirikisha Zuchu iliyomaliza mwaka 2022 na views milioni 22 tu.

Rema ambaye alijiunga YouTube Aprili 7, 2019 ikiwa ni miaka minane baada ya Diamond, amefikisha jumla ya 'views' milioni 991 ndani ya miaka minne tu ikiwa ni karibia nusu ya 'views' za Diamond alizokusanya kwa miaka 12.
Kwa upande wake AyraStar ambaye ni msanii chipukizi Nigeria, hivi karibuni video ya wimbo wake 'Rush' iliyotoka Septemba 26, 2022 tayari imefikisha 'views' milioni 117 YouTube ikiwa ni miezi mitano tangu kuachiwa, hizi ni rekodi za solo ambazo Diamond hana!

Ikumbukwe mwaka 2019 Yemi Alade aliandika rekodi kama mwimbaji wa kwanza wa kike Afrika kufikisha 'views' milioni 100 YouTube, ni kupitia video ya wimbo wake, Johnny iliyotoka Machi 3, 2014.

Katika orodha ya video 10 za muziki zilizotazamwa zaidi YouTube Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa muda wote, hakuna video hata moja ya Diamond.

Mwisho.

#avmediaupdates #avmediainfos #breaknews #radio #vpl #epl #tmz #netflix #tv #youtube #habari #bongofleva #bongomovie #muziki #movie #Tanzania #Kenya #uganda #burundi #rwanda

Comments

Popular posts from this blog

Lavalava kujiunga na Aftermath Entertainment na kuondoka WCB

Kundi la Sauti Soul Kuvunjika

BAADA YA KUWA ‘MNYONGE SANA’ …PHIRI KUWA CHINI YA UANGALIZI MAALUMU SIMBA