Kipi kinamkwamisha Lavalava WCB


 Hata hivyo, sasa inaonekana kuna kitu hakipo sawa kwa Lava Lava katika safari yake ya muziki ukilinganisha na wasanii wengine hasa wale waliokuja nyuma yake, Mbosso na Zuchu.


Mbosso aliyejiunga WCB Wasafi, Januari 2018, tayari ametoa albamu moja, Definition of Love (2021) na EP moja, Khan (2022), wakati Lava Lava ametoa EP moja tu, Promise (2021).

Tayari Mbosso ameshinda tuzo mbili, HiPipo Awards 2019 kama Video Bora ya Mwaka (Hodari) na Tanzania Music Awards (TMA) 2022 kama Msanii Bora wa Kiume wa Bongofleva, ila Lava Lava hajashinda tuzo yoyote.

Naye Zuchu aliyetambulishwa WCB Wasafi hapo Aprili 2020 katoa EP moja, I Am Zuchu (2020) sawa na Lava Lava lakini yake ilitoka kwa ukubwa zaidi, ilifanyiwa 'listenig party', huku akitoa video tano wakati ile ya Lava Lava ikitoa video moja tu!.

Wakati mwaka huu Zuchu akiandika rekodi kama msanii wa kike Bongo aliyeshinda tuzo nyingi za TMA 2022, tano, Lava Lava hata hakuchaguliwa kuwania, ni yeye na Queen Darleen pekee ndio wasanii wa WCB Wasafi waliokosa tuzo hizo.

Hata upande wa mauzo wa kazi zao mtandaoni wanaonekana kumzidi, mfano Mbosso na Zuchu ndio waliotangulia kufikisha wafuasi (subscribers) zaidi ya milioni 1 YouTube wakati Lava Lava aliwatangulia kimuziki chini ya WCB Wasafi.

Kwenye mitandao ya kijamii, mfano Instagram, Lava Lava ndiye msanii wa WCB Wasafi mwenye namba ndogo zaidi ya wafuasi (followers) akiwa nao milioni 3.6, hata wale waliomkuta wamemzidi, Mbosso (milioni 6) na Zuchu (milioni 5.6).

Inaendelea....!

#avmediaupdates #avmediainfos #breaknews #radio #vpl #epl #tmz #netflix #tv #youtube #habari #bongofleva #bongomovie #muziki #movie #Tanzania #Kenya #uganda #burundi #rwanda

Comments

Popular posts from this blog

Lavalava kujiunga na Aftermath Entertainment na kuondoka WCB

Kundi la Sauti Soul Kuvunjika

BAADA YA KUWA ‘MNYONGE SANA’ …PHIRI KUWA CHINI YA UANGALIZI MAALUMU SIMBA