Posts

Hii Hapa ni Jumla ya Fedha Watakazovuna Yanga Baada ya Kuingia fainali

Image
YANGA tayari ipo kwenye fainali za Shirikisho Afrika, baada ya kuwatoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini wiki hii. Mabingwa hao wa Tanzania, wamejikakikishia kiasi cha Dola 800,000 (zaidi ya Sh 1.8 Bilioni) kwa kutinga fainali na kama itafanikiwa kuinyoosha USM Alger ya Algeria watakaokutana nao basi, itazoa Dola 2 Milioni (zaidi ya Sh 4.7 Bilioni). Lakini kama unadhani Yanga itavuna kiasi hicho tu, pole yako kwani kwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa pili mfululizo, tayari wababe hao wameshajihakikisha zaidi ya Sh 700 milioni kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo yaani Benki ya NBC na Azam Media. Azam inayodhamini matangazo ya ligi hiyo bonasi zake kwa bingwa wa msimu ni Sh 500 milioni, huku kwa NBC wanatoka Sh 100 milioni ilihali wadhamini wakuu wa Yanga, SportPesa inayoipa klabu hiyo zaidi ya Sh 4 Bilioni kwa mujibu wa mkataba mpya walioingia mwaka jana wenye thamani ya Sh 12 Bilioni kwa miaka mitatu, pia itaipa mabingwa hao Sh 150 Milioni kama bonasi ya ubingwa. Ukiacha fe

Lavalava kujiunga na Aftermath Entertainment na kuondoka WCB

Image
Hakuna ubishi kuwa baada ya Mbosso na Zuchu kusainiwa kulipelekea WCB Wasafi kupunguza nguvu kwa baadhi ya wasanii ambao ni Lava Lava na na Queen Darleen. Mathalani ni zaidi ya miaka mitatu sasa Queen Darleen hajatoa wimbo, mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa Aprili 2020 alipoachia ngoma, Bachela akimshirikisha Lava Lava, huku akiwa hajatoa albamu wala EP chini ya WCB Wasafi. Ujio wa wageni hao wawili hasa Zuchu, kunaweza kutafsiriwa kama kutia mchanga kitumbua cha Lava Lava, mfano Zuchu amekuwa anatoa ngoma mfululizo kuliko msanii yoyote wa WCB Wasafi. Wakati Lava Lava anatimiza miezi tisa bila kutoa ngoma, kwa kipindi hicho Zuchu ameweza kutoa ngoma sita ambazo ni Jaro, Love, Kwikwi, Utaniua, Napambana na Nani. Kwa mwenendo huo huwenda maisha ya Lava Lava sio marefu ndani ya WCB Wasafi, anaweza kuondoka kama ilivyokuwa kwa Harmonize, Rich Mavoko na Rayvanny. Hata hivyo, swali la wengi ni vipi ataweza kupata mafanikio kuzidi yale aliyopata chini ya lebo hiyo? au ataenda kuwa tishio k

Diamond Platnnumz, Alikiba, Harmonize, Sauti Sol Waletewa tuzo zao

Image
  Waandaaji wa Tuzo za Magic Vibes Awards wamezungumza na wana habari leo wakieleza kuleta tuzo kwa wasanii walioshinda baada ya kutangazwa washinndi. Tuzo hizo ambazo zinaanndaliwa nchini Marekani Texas ni maalumu kwa ajili ya wasanii kutoka Afrika Mashariki. Miongoni mwa wasanii walioshiriki ni Diamond Platnnumz, Alikiba, Harmonize, Sauti Sol na wengine.

Kundi la Sauti Soul Kuvunjika

Image
Kundi la muziki kutokea nchini Kenya, Sauti Sol limetangaza kuwa litavunjika kwa muda mara baada ya kumalizika kwa ziara yao ya kimataifa. Katika taarifa yake kwa umma Jumamosi hii, wamesema ziara yao katika nchi za Marekani, Ulaya na Canada ni fursa kwa mashabiki wao kujumuika nao kwa mara ya mwisho. cc  @sautisol #avmediaupdates   #avmediainfos   #breaknews   #radio   #vpl   #epl   #tmz   #netflix   #tv   #youtube   #habari   #bongofleva   #bongomovie   #muziki   #movie   #Tanzania   #Kenya   #uganda   #burundi   #rwanda  

Kipi kinamkwamisha Lavalava WCB

Image
  Hata hivyo, sasa inaonekana kuna kitu hakipo sawa kwa Lava Lava katika safari yake ya muziki ukilinganisha na wasanii wengine hasa wale waliokuja nyuma yake, Mbosso na Zuchu. Mbosso aliyejiunga WCB Wasafi, Januari 2018, tayari ametoa albamu moja, Definition of Love (2021) na EP moja, Khan (2022), wakati Lava Lava ametoa EP moja tu, Promise (2021). Tayari Mbosso ameshinda tuzo mbili, HiPipo Awards 2019 kama Video Bora ya Mwaka (Hodari) na Tanzania Music Awards (TMA) 2022 kama Msanii Bora wa Kiume wa Bongofleva, ila Lava Lava hajashinda tuzo yoyote. Naye Zuchu aliyetambulishwa WCB Wasafi hapo Aprili 2020 katoa EP moja, I Am Zuchu (2020) sawa na Lava Lava lakini yake ilitoka kwa ukubwa zaidi, ilifanyiwa 'listenig party', huku akitoa video tano wakati ile ya Lava Lava ikitoa video moja tu!. Wakati mwaka huu Zuchu akiandika rekodi kama msanii wa kike Bongo aliyeshinda tuzo nyingi za TMA 2022, tano, Lava Lava hata hakuchaguliwa kuwania, ni yeye na Queen Darleen pekee ndio wasanii w