Simba Pengine hizi zitabaki kuwa ni fikra zangu tu! Lakini yote ilikuwa ni usajiri tu! Ukiitizama Yanga SC ambayo iliwachukuwa takribani miaka 5 hadi 4 kurudi katika ubora wake na kushinda mataji mbele ya Simba na Azam, ilikuwa ni usajiri tu! Kipindi kile Simba anashinda mataji ya Ligi Kuu Mara 4 mfululizo mbele ya Yanga SC, ilikuwa ni usajili tu! Kule Yanga kulikuwa na usajili usiyoendana na ukubwa wa klabu, pia ulikuwa haulingani ubora na mahasimu wao ambao ni Simba wakionekana ni bora kila idara na kushinda mataji mara 4 kwa sababu Simba walikuwa na usajiri bora kuliko watani zao Yanga, ilikuwa ni usajiri tu! Simba kulikuwa na akina kachi kahata, Louis Miquissone, Chama, Meddie Kagere, John Bocco, Hassan Dilunga, Emmanuel Okwi, Deo Kanda, Gyan na wengine. Wote wakiwa kwenye ubora na wakiitumikia Simba kwa faida kubwa, wengine wakauzwa, wengine wakabaki, na wengine wakaachwa, yote ilikuwa ni usajiri tu! Kule Yanga kulikuwa na akina Sadney Urikhob, Lamine Moro, Juma Balinya, Yikpe, D